ZANZIBAR-Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema, Serikali inatoa mkopo kwa asilimia 100 kwa wanafunzi wanaofaulu zaidi masomo ya sayansi kidato cha sita na kusomea nyanja za Sayansi, Elimu Tiba, Uhandisi, Hisabati na TEHAMA Elimu ya Juu.
Prof.Mkenda amesema hayo Agosti 24, 2024 baada ya kuzindua Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Dimbani na Dahalia ya Wanafunzi wa kike katika skuli hiyo kisiwani Unguja, akiwasisitiza walimu kuwahimiza wanafunzi kutumia fursa hiyo kikamilifu.