Prof.Nombo akutana na wadau wa elimu kutoka ADEA

DODOMA-Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Prof. Carolyne Nombo leo Agosti 12, 2024 jijini Dodoma amekutana na wadau wa elimu kutoka Chama cha Maendeleo ya Elimu barani Afrika (ADEA) kwa ajili ya kutambulisha Mradi wa Ukusanyaji wa Takwimu za Elimu na Ustadi.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Prof. Carolyne Nombo akiteta na wadau wa elimu kutoka Chama cha Maendeleo ya Elimu barani Afrika (ADEA) leo Agosti 12, 2024 jijini Dodoma.

Ujumbe huo umemweleza Katibu Mkuu kuwa mradi huo utafanya kazi katika nchi 30 za Afrika kwa kipindi cha miaka mitano ukiwa na lengo la kuandaa na kukusanya taarifa zenye ubora ili kufanikisha ufuatiliaji wa maendeleo ya elimu.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Prof. Carolyne Nombo akiteta na wadau wa elimu kutoka Chama cha Maendeleo ya Elimu barani Afrika (ADEA) leo Agosti 12, 2024 jijini Dodoma.

Prof. Carolyne Nombo ameridhishwa na Mradi huo kwa kuwa Tanzani imeanza utekelezaji wa mitaala na Sera mpya ya elimu na kwamba Mradi huo utasaidia na kuwa chachu ya kukusanya Taarifa za wanafunzi kuanzia ngazi ya Elimu ya Awali, Elimu ya Juu mpaka katika soko la ajira.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Prof. Carolyne Nombo akiteta na wadau wa elimu kutoka Chama cha Maendeleo ya Elimu barani Afrika (ADEA) leo Agosti 12, 2024 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu amewataka wajumbe hao kutembelea Taasisi mbalimbali zinazojihusisha na masuala ya ukusanyaji wa Taarifa ikiwemo Taasisi kama (e-GA) Mamlaka ya Serikali Mtandao, NBS | Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Eastern Africa Statistical Training Center (EASTC) na Chuo Kikukuu cha Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news