ZANZIBAR-Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo tarehe 26 Agosti,2024 amekutana na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bw. Khamis Abdulla Said kuona namna ya kuimarisha ushirikiano baina ya Wizara hizo mbili katika masuala ya Elimu ikiwemo Sayansi, Teknolojia na Ubunifu.
Katika mazungumzo hayo Prof. Nombo ameambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Teknolojia, Prof. Ladislaus Mnyone.