Rais Dkt.Mwinyi aitaka jamii kuweka mkazo maadili ya watoto na vijana

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameitaka jamii kuweka mkazo katika malezi ya watoto na vijana ili kuwanusuru na mmomonyoko wa maadili.
Alhaj Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Agosti 23, 2024 alipotoa salamu baada ya kushiriki katika sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Shuraa uliopo Magomeni, Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.
Ameeleza kuwa, kumekuwa na mmomonyoko mkubwa wa maadili na vitendo viovu vinavyosababishwa na vijana kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya na unywaji wa pombe uliokithiri.

Pia,Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinhi amewahimiza wazazi kuhakikisha vijana wanapata elimu ya dini kwa ajili ya kujitambua na kujiepusha na vitendo viovu.
Alhaj Dkt. Mwinyi ameongeza kuwa, Zanzibar ilikuwa nchi yenye sifa katika kusimamia maadili, lakini yameporomoka kutokana na matumizi ya dawa za kulevya kwa kundi kubwa la vijana.

Aidha, amewahimiza viongozi wa dini kuendelea kuhubiri na kuwahimiza waumini kufuata misingi ya dini ili kuirejesha nchi katika maadili mema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news