Rais Dkt.Mwinyi aridhika na kazi za UVCCM

ZANZIBAR-Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema,Chama cha Mapinduzi kinaridhishwa na kazi zinazofanywa na Umoja wa Vijana UVCCM.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar akizungumza na wajumbe wa Baraza la UVCCM Taifa Agosti 11,2024 Ikulu jijini Zanzibar.

Ameeleza kuwa,ni vyema kile kinachofanywa na umoja huo kiwe changamoto kwa jumuiya nyingine za chama ili kuyafikia malengo.Dkt.Mwinyi ameyasema hayo Agosti 11,2024 wakati akizungumza na wajumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa Ikulu Zanzibar alipowaalika kwa chakula cha jioni.
Makamu Mwenyekiti Dkt. Mwinyi amewahakikishia vijana kuwa, Serikali inajipanga kuendelea kujenga viwanja zaidi vya Michezo hapa nchini ili kuinua Vipaji vya Vijana.

Amewasisitiza kutochokozeka na propaganda za wapinzani na kuwahimiza kuhubiri Amani , upendo na Umoja wakati wote.
Naye Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndugu, Jokate Mwegelo amesema Vijana wana wajibu wa kuacha alama katika Chama kutokana nyadhifa wanazopatiwa na Taifa.

Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Mohamed Kawaida ameeleza kuwa mwitikio wa kampeni ya kijana na kijani imetoa Dira na muelekeo wa namna gani UVCCM itaingia katika Uchaguzi kuipatia CCM ushindi wa kishindo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news