Rais Dkt.Mwinyi ashiriki Nishani za miaka 60 ya JWTZ

DAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameshiriki hafla ya kutunuku Nishani ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ambayo imeongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Rais Dkt. Samia amewatunuku nishani hizo akiwemo Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF) Jenerali Jacob John Mkunda, Majenerali, Maafisa pamoja na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 29, 2024.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar, viongozi wa Serikali, Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na viongozi wa Dini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news