Rais Dkt.Mwinyi atoa maelekezo kwa TAKUKURU na ZAECA

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amezisihi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) kuongeza ushirikiano kwenye ufanisi wa kazi zao.
Dkt. Mwinyi ametoa nasaha hizo leo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Francis Chalamila aliyefika kujitambulisha kufuatia uteuzi wa kutumikia nafasi aliyonayo uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.

Rais Dkt. Mwinyi amezishauri taasisi hizo mbili kuzidisha ushirikiano hasa kwenye miradi ya kimkakati ya Mendeleo kwa maslahi ya taifa.

Aidha, Dkt. Mwinyi amempongeza Mkurugenzi Chalamila kwa uteuzi alioupata na kumtakia heri kwenye majukumu yake mapya.

Pia, Rais Dkt. Mwinyi amesifu jitihada za ZAECA kwa kuendeleza ufanisi wa makujukumu yao hasa kwenye miradi ya Serikali kwa wanawajibika ipasavyo.
Akizungumza kwa wakati huo, Bw. Chalamila amemuahidi Rais Dkt. Mwinyi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya ZAECA na TAKUKURU katika kufanikisha majukumu yanayowalazimu.

Amesema, TAKUKURU na ZAECA wanashirikiana kwenye mambo mengi tokea waliposaini mkataba wa ushirikiano wao mwaka 2012, ikiwemo kujengeana uwezo, kusihirikana kwenye masuala ya uchunguzi wa kazi zao, kushiriki mikutano ya pamoja ya kikanda na kitaifa.

Vile vile,Bw. Chalamila amesifu na kupongeza juhudi za maendeleo makubwa zilizofikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Dk. Mwinyi.

Alisema, mbali na majukumu mengine walivyonayo TAKUKURU na ZAECA imekua rahisi kwao kushirikiana hasa kuwadhibiti wahalifu wa pande mbili za Muungano wanaojaribu kukimbilia kwenye mipaka ya sehemu hizo Bara na Visiwani.
Bw. Chalamila pia alimuahidi Rais Dk. Mwinyi na Rais Dkt. Samia kuendeleza maono yao, na ushauri wao katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa na uhujumu uchumi kwa kushirikiana na ZAECA.

Sambamba na kuendeleza mikakati na uchunguzi kwenye miradi ya maendelo na kumuhakikishia Rais Dk. Mwinyi kwamba wataendelea kusimamia miradi hiyo na kuhakikisha inakamilika kwa viwango vinavyostahiki na kuhakikisha thamani ya fedha za miradi hiyo inaonekana.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alimteua Bw. Chalamila kushika wadhifa alionao sasa Agosti 14 mwaka huu na kumuapisha Agosti 15, mwaka huu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news