Rais Dkt.Mwinyi awaapisha makatibu wakuu wapya

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe. Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewaapisha makatibu wakuu wa wizara mbalimbali aliowateua hivi karibuni.
Ni kupitia hafla iliyofanyika leo Agosti 24, 2024 IKULU jijini Zanzibar. Walioapishwa kuwa makatibu wakuu ni;
1.Dkt.Habiba Hassan Omar ameapishwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi.

2.Dkt.Mngereza Mzee Miraj ameapishwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya.

3.Ndugu Maryam Juma A.Saadalla ameapishwa kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais.

4 .Ndugu Khamis Suleiman Mwalim ameapishwa kuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Kazi ,Uchumi na Uwekezaji.

Hafla hiyo ya uapisho imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Dini na Vyombo vya ulinzi na Usalama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news