Rais Dkt.Mwinyi awasili nchini Indonesia

BALI-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ngurah Rai jijini Bali, Indonesia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Indonesia na Afrika pamoja na Mkutano wa Viongozi kujadili ubia wa Maendeleo unaoanza kesho Septemba 1 hadi 3, 2024.
Rais Dkt. Mwinyi na ujumbe wake wamepokelewa na Naibu Waziri wa Biashara wa nchi hiyo, Dkt. Jerry Sambuaga, pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Indonesia, Mheshimiwa Makocha Tembele.
Rais Dkt. Mwinyi ameambatana na mkewe, Mama Mariam Mwinyi, akiwa nchini Indonesia, atafanya pia ziara ya kikazi ambayo itaanzia Bali na kumalizia jijini Jakarta.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news