ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema,Serikali itaendelea kuwekeza zaidi katika sekta ya elimu kwa kujenga miundombinu bora na kuboresha maslahi ya walimu ili mafanikio yanayopatikana yaongezeke kila mwaka.


Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kufarijika kwake na mafanikio yaliyopatikana, ikiwemo ongezeko la idadi ya wanafunzi waliopata daraja la kwanza.
Aidha, amesisitiza kuwa Serikali itaweka kipaumbele kuimarisha miundombinu, kuajiri walimu zaidi hasa kwa masomo ya sayansi, na kusimamia maslahi ya walimu ili kuwaongezea motisha ya kufanya kazi kwa ufanisi.
Rais Dkt. Mwinyi amefahamisha kuwa Serikali inakusudia kuongeza fedha za mikopo kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya juu, na ametoa wito kwa wanafunzi kutumia fursa hiyo kujiendeleza zaidi.