Rais Dkt.Samia akutana na Mwalimu wake Chuo Kikuu Mzumbe

MOROGORO-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan leo Agosti 4,2024 amekutana na mwalimu wake wa Chuo Kikuu Mzumbe mkoani Morogoro,Mama Sabina Gellejah.
Hili ni kati ya tukio ambalo licha ya kurejesha kumbukizi nzuri kati ya mwalimu na mwanafunzi wake, pia limeonesha heshima kubwa kwa walimu ikizingatiwa kuwa, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia mbali na kuzipa kipaumbele sekta mbalimbali za uchumi nchini, pia elimu wakiwemo walimu wamekuwa waakineemeka kupitia uongozi wake.
"Nimefurahi kukutana na mmoja wa waliokuwa waalimu wangu nikiwa mwanafunzi wa IDM Mzumbe (sasa Chuo Kikuu Mzumbe) kuanzia mwaka 1983 hadi 1986 Mama Sabina Gellejah, baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Majengo ya Kampasi Mpya ya Chuo Kikuu Mzumbe."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news