Rais Dkt.Samia amkabidhi Waziri Ridhiwani Kikwete vyeti kwa kutambua mchango wa NSSF na WCF kurudisha kwa jamii

ZANZIBAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan amemkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete vyeti vya kutambua mchango wa mashirika mawili yaliyopo chini ya wizara yake.
Mashirika hayo ni Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa mchango wao katika kurudisha kwa jamii.
"Mashirika haya yamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha yanajenga na kuwezesha jamii ambayo inaondoka katika utegemezi kwenda kwenda kujitegemea.
"Kupitia kazi zao na mapato yao, jamii imeendelea kufaidia kwa kazi na matokeo mbalimbali ususani uwekezaj mkubwa unaofanyika. Kazi nzuri inatambuliwa na inaiheshimisha jamii yetu,"amesisitiza Mheshimiwa Waziri Ridhiwani Kikwete.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news