Rais Dkt.Samia apokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Guinea nchini mwenye Makazi yake Ethiopia

DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amepokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Guinea hapa nchini mwenye Makazi yake Addis Ababa nchini Ethiopia,Mhe. Nounke Kaba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Guinea hapa nchini mwenye Makazi yake Addis Ababa nchini Ethiopia Mhe. Nounke Kaba, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Agosti, 2024.
Balozi Mteule wa Guinea hapa nchini mwenye Makazi yake Addis Ababa nchini Ethiopia, Mhe. Nounke Kaba akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam kuwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan tarehe 13 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Guinea hapa nchini mwenye Makazi yake Addis Ababa nchini Ethiopia, Mhe. Nounke Kaba. Ni baada ya Balozi huyo kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mheshimiwa Rais Dkt.Samia.
Balozi Mteule wa Guinea hapa nchini mwenye Makazi yake Addis Ababa nchini Ethiopia Mhe. Nounke Kaba akiwa amesimama (katikati) pamoja na viongozi wengine wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania ukipigwa kabla ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Suluhu Samia. Ni Agosti 13,2024 Ikulu jijini Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news