Rais Dkt.Samia ataka Wizara ya Nishati kuongeza kasi usimamizi wa miradi

MOROGORO-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Nishati kuongeza nguvu katika kusimamia miradi yote ya nishati ili ikamilike kwa wakati na hivyo kuwawezesha wananchi kupata nishati ya uhakika.
Rais Samia ametoa agizo hilo Agosti 06, 2024 wakati akihitimisha ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro.
"Nimejionea mwenyewe wakati naenda Kilosa tofauti iliyokuwa ikionekana maeneo ambayo hayana umeme na yale yenye umeme ambayo yameshamiri kwa shughuli za biashara, hii inaonesha umuhimu wa nishati katika maeneo yote nchini."

Aidha, Rais Samia ameutaka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kukamilisha mapema kupeleka umeme kwenye Vijiji vilivyobaki na kuongeza kasi ya kusambaza umeme kwenye Vitongoji ili wananchi waweze kufanya kazi za maendeleo
Aidha, amesisitiza kuwa uwepo wa umeme wa uhakika kutoka Bwawa la Julius Nyerere kunaufanya Mkoa wa Morogoro kuwa sehemu sahihi ya uwekezaji.

"Morogoro sasa ina umeme wa uhakika, hali inayovuta uwekezaji ndani ya mkoa."
Akizungumzia kuhusu miradi ya umeme vijijini Mkoa wa Morogoro, Dkt. Samia amesema kupitia Wakala wa Nishati Vijijini Serikali imepeleka umeme kwenye Vijiji 621 kati ya Vijiji 669.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news