DODOMA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Kilimo kuisimamia kwa ukaribu Sekta ya Ushirika ili uwekezaji unaofanywa na Serikali kwenye sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi uweze kufanywa na Vyama vya Ushirika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na maafisa ugani na wanaushirika Ikulu Chamwino jijini Dodoma leo Agosti 10, 2024.
Rais Dkt.Samia ametoa agizo hilo leo Agosti 10,2024 katika kikao na Maafisa Ugani na wanaushirika kilichofanyika Ikulu, Chamwino jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na maafisa ugani na wanaushirika Ikulu Chamwino jijini Dodoma leo Agosti 10, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na maafisa ugani na wanaushirika Ikulu Chamwino jijini Dodoma leo Agosti 10, 2024.
Aidha, Rais Dkt. Samia amesema Serikali ina dhamira ya kurudisha hadhi ya ushirika
hususan ushirika wa mazao hivyo ametaka Ushirika uendeshwe kisasa, uwekezaji ufanywe
kitaalam na ukiwa na lengo la kumnufaisha mwanaushirika moja kwa moja.
Vile vile, Rais Dkt. Samia amevitaka Vyama vya Ushirika kutokuwa sehemu ya kumyonya
mwanaushirika, bali viwe mstari wa mbele kuwalinda na kuwatetea.
Rais Dkt. Samia pia amevielekeza Vyama vya Ushirika kuwa chachu ya mabadiliko na vyenye
kuleta mageuzi ya fikra, ikiwemo kuchangia maendeleo mapana kwa kuhamasisha wanaushirika waweze kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii na Mfuko wa Bima ya Afya kwa wote.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na maafisa ugani pamoja na wanaushirika kabla ya kuanza kwa kikao na maafisa hao Ikulu Chamwino jijini Dodoma leo Agosti 10, 2024.

Rais Dkt. Samia ameagiza Maafisa Ugani na Maafisa Ushirika kuhakikisha kuwa ruzuku ya
pembejeo inayotolewa na Serikali inaleta matokeo makubwa zaidi, kuwafikia wananchi
vijijini pamoja na kuwaelimisha mbinu bora za kilimo, ufugaji na uvuvi.
Kwa upande mwingine, Rais Dkt. Samia ameitaka Wizara ya Kilimo kuandaa utaratibu wa kuwapima Maafisa Ugani kwa tija inayozalishwa kwenye Kata au Kijiji anachokisimamia ili uwekezaji unaoufanywa na Serikali utoe matokeo yanayotarajiwa.
Hali kadhalika, Rais Dkt. Samia amewataka Maafisa Ugani katika ngazi ya Kata kukaa kwenye vituo vyao na kutumia usafiri ambao Serikali imewapatia kuwafikia na kuwahudumia wananchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waandishi wa Habari kutoka mkoa wa Dodoma muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao na maafisa ugani pamoja na wanaushirika Ikulu Chamwino jijini Dodoma leo Agosti 10, 2024.

Rais Dkt. Samia ameeleza kuwa Serikali itaunga mkono juhudi za wanaushirika kuanzisha Benki ya Ushirika ya Taifa kwa kuchangia shilingi bilioni 5 kama mtaji ili kuwezesha shughuli za benki hiyo kuanza.