DODOMA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameutaka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), kuhakikisha wanawafikia wananchi wote ili wawe ndani ya mfumo wa Bima ya afya.

Ameyasema hayo leo wakati akitembelea maonesho ya Nane Nane kitaifa mkoani Dodoma.
Hivi karibuni Mhe. Rais akiwa ziarani mkoani Katavi na Rukwa kwa nyakati tofauti alihamasisha wananchi kukata bima ya afya ili wawe na uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wote.
Tags
Bima ya Afya kwa Wote
Dr Samia Suluhu Hassan
Habari
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)
NHIF Tanzania