DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan amewaapisha mawaziri na baadhi ya viongozi aliowateua Agosti 14,2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwaapisha Mawaziri kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam leo tarehe 15 Agosti, 2024. Mawaziri hao walioapa ni: Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (Mb.) kuwa Waziri wa Katiba na Sheria; Mhe. William Vangimembe Lukuvi (Mb.) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu); Mhe. Jenista Joackim Mhagama (Mb.) kuwa Waziri wa Afya; na Mhe. Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana (Mb.) kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Hamza Johari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Samwel Marco Maneno kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Abdul Rajab Mhinte kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Bw. Atupele Webster Mwambene kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshugulikia masuala ya Elimu, kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Dkt. Ally Saleh Possi kuwa Wakili Mkuu wa Serikali kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Bw. Crispin Francis Chalamila kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Agosti, 2024.