KIGALI-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali nchini Rwanda,tayari kwa kuhudhuria sherehe za uapisho wa Rais mteule wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame leo Agosti 11, 2024.


