DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Agosti 29,2024 Ukumbi wa Jakaya Kikwete uliopo Ikulu jijini Dar es Salaam ametunuku Nishani ya miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa maafisa mbalimbali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwatunuku Nishani ya miaka 60, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF) Jenerali Jacob John Mkunda, Majenerali, Maafisa pamoja na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Viongozi mbalimbali kwenye hafla ya kutunuku Nishani ya miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Agosti, 2024.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya kutunuku Nishani ya miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 29 Agosti, 2024.