DODOMA-Rais mpya wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS, Boniface Mwambukusi ameapishwa rasmi kuongoza chama hicho kwa miaka mitatu ijayo.

Mwabukusi alitangazwa mshindi wa kiti hicho na Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mawakili Agosti 2,2024 kwa kupata kura 1,274 ambazo ni sawa na asilimia 63.1 dhidi ya washindani wake Sweetbert Nkuba, Revocutus Kuuli, Ibrahim Bendera, Paul Kaunda na Emmanuel Muga katika uchaguzi ambao kwa mara ya kwanza umefanyika nje ya Jiji la Arusha