RC wa Mara atoa wiki sita kwa DED wa Serengeti

MARA-Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Alfred Mtambi ametoa wiki sita kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kukamilisha bweni la wanafunzi wa kidato cha tano.
Ni katika Shule ya Sekondari Ngoreme lilojengwa kwa nguvu za wananchi na wanafunzi waliosoma katika shule hiyo.

Mtambi ametoa kauli hiyo alipofanya ziara wilayani Serengeti mkoani humo ambapo shule hiyo tayari imepangiwa wanafunzi.

Kutokana na changamoto hiyo, kwa sasa wanafunzi wanalazimika kulala kwenye madarasa mawili,hivyo kumlazimu kuagiza kukamilisha Bweni hilo ili lianze kutumika.

Bweni hilo la wanafunzi wa kidato cha tano lilijengwa na kuwekewa jiwe la msingi mwaka 2017 kwa gharama ya shilingi milioni 78.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news