REA yatekeleza dhamira ya Rais Dkt.Samia kwa vitendo

✔️Yaendelea kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia

DODOMA-Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Mdau Lake Gas Limited imetoa ofa maalum kipindi hiki cha Maonesho ya Nanenane ya kuuza mitungi midogo ya gesi kwa shilingi 22,400 badala ya Sh. 44,800 kwa lengo kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.Ofa hiyo maalum imetangazwa rasmi Agosti 5, 2024 na Afisa Upimaji Mwandamizi wa Wakala wa Nishati Vijijini, Hussein Shamdas katika Banda la Wakala ndani ya viwanja vya Maonesho ya Nane Nane, Nzuguni Jijini Dodoma.
"Tunaendelea kushirikiana na wadau kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya kupikia, na katika Maonesho haya tumekuja na Ofa maalum ya kuuza mitungi ya gesi kwa shilingi elfu ishirini na mbili na mia nne tuu," amesema Shamdas

Amesema Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 ambao ulizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan mnamo Mwezi Mei mwaka huu umelenga kuhakikisha kuwa 80% ya Watanzania wanatumia nishati hiyo ifikapo mwaka 2033.
"Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonyesha njia, nasi tunatekeleza kuhakikisha lengo la 80% linafikiwa," amesema Shamdas.

Amebainisha kuwa Wakala unashirikiana kwa karibu na wadau mbalimbali katika kufikia azma hiyo ya kuongeza matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwa kutumia teknolojia rafiki na ya kisasa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news