Samia Scholarship inahamasisha usomaji fani za Sayansi-Waziri Prof.Mkenda

ZANZIBAR-Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema uwepo wa Samia Scholarship imekuwa ni kivutio kuwahamasisha wanafunzi wenye uwezo mkubwa katika Sayansi kuendelea kusomea fani za Sayansi ambazo zinalenga kuchochea ustawi na maendeleo ya Taifa.
Akizungumza Agosti 26, 2024 katika hafla ya kuwapongeza wanafunzi waliopata daraja la Kwanza katika Mtihani wa Kidato cha nne na sita Visiwani Zanzibar, Waziri Mkenda ameeeleza pis kuwa fursa za mikopo ya Elimu ya Juu zinatolewa kulingana na ufaulu wa Mwanafunzi.

"Katika kutekeleza ilani ya CCM na maelekezo ya Rais, Serikali Samia Skolashipu inatoa ufadhili asilimia mia moja wanaosomea nyanja za Uhandisi, Elimu Tiba, Sayansi, Hisabati na TEHAMA na niwahakikishie Mikopo inatolewa kwa kufuata vigezo vilivyowekwa," amesema Prof.Mkenda.

Amebainisha kuwa, Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ameongeza fedha za mikopo kutoka Bilioni 464 hadi Bilioni 757 na kwamba zitaendelea kuongezeka ili kuwezesha wanafuzi wengi wenye vigezo kupata elimu ya juu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news