Serikali imetenga shilingi bilioni 31.8 kuwawezesha wananchi-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema,tayari Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 31.8 kupitia Wakala wa Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi, ikiwemo kuwawezesha vijana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika maadhimisho ya kilele cha Siku ya Vijana Kimataifa 2024, yaliyofanyika Agosti 12,2024 Golden Tulip Hotel, Airport, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.

Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amesema,tayari shilingi milioni 338.6 zimetolewa kwa makundi mbalimbali.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo Agosti 12,2024 katika maadhimisho ya kilele cha Siku ya Vijana Kimataifa 2024, yaliyofanyika Golden Tulip Hotel, Airport, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.
Aidha, Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa tayari vijana 500,000 wanaendelea kupata mafunzo ya stadi za maisha, mafunzo ya matumizi ya TEHAMA, na ujasiriamali.

Rais Mwinyi ameridhia maombi yaliyotolewa na vijana katika maadhimisho hayo, ikiwa ni pamoja na kuzingatia suala la maendeleo ya vijana katika mipango yao na kuongezwa kwa bajeti ya wizara katika masuala yanayohusu vijana na taasisi za mikopo ili kuwawezesha vijana kupata mikopo kwa wepesi na kwa urahisi.
Aidha, Dkt. Mwinyi amewataka vijana kushiriki kwa wingi na kugombea katika uchaguzi mkuu ujao na kuahidi kuongeza idadi ya vijana katika uteuzi wa nyadhifa mbalimbali Serikalini.

Naye, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita amesema juhudi zinaendelea za kuimarisha vituo vya stadi za maisha na tayari Serikali imetenga shilingi bilioni 4.5 kwa ajili ya ujenzi wa kituo kikubwa cha kuwawezesha vijana.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news