NA VERONICA MWAFISI
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu amesema kuwa msingi mkuu wa ufanyaji kazi wa Serikali ni kwa kupitia nyaraka ambazo zinaisaidia Serikali kutimiza uwajibikaji katika kutekeleza majukumu yake kupitia miongozo ya nyaraka hizo.

Naibu Waziri Sangu amesema kuwa utunzaji wa nyaraka kupitia Idara hiyo ni jukumu adhimu linalohitaji viwango vikubwa vya usimamizi ili kuleta haki na uwazi katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya Serikali kwa kutumia nyaraka hizo.
Aidha Mhe. Sangu ameipongeza Idara hiyo kwa namna wanavyofanya kazi kubwa ya kuwaenzi waasisi wa Taifa la Tanzania kwa kukusanya na kutunza kumbukumbu zao zitakazosaidia vizazi vijavyo kufahamu historia ya nchi kupitia waasisi hao.

