Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi binafsi za elimu-Mheshimiwa Kapinga

RUVUMA-Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema, Serikali itaendelea kuwaunga mkono na kushirikiana na wadau wote wa elimu nchini ili kutimiza lengo la kufikisha elimu stahiki kwa makundi yote ya wananchi mijini na vijijini.
Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Agosti 17, 2024 wakati wa Maadhimisho ya Miaka 25 ya kusajiliwa kwa Shule ya Msingi Huruma inayomilikiwa na Kanisa Katoliki wilayani Mbinga mkoani Ruvuma.
"Uwepo wa shule kama hii unadhihirisha jinsi mnavyoiunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita katika kutoa elimu bora kwa watanzania, nitumie fursa hii kulipongeza Kanisa Katoliki kwa kuendelea kuwa mdau mkubwa wa Serikali katika huduma za kijamii kama afya, elimu na huduma nyinginezo."

Kuhusu shule hiyo ya Hekima amesema kuwa, Serikali inatambua mchango wa shule hiyo hasa kwa kutoa huduma kwa watoto wenye mahitaji maalum.
Mhe. Kapinga pia amewaasa wanafunzi kuwa waaminifu pamoja na kujitolea katika kusaidia wengine.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news