ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa Serikali itaendelea kuwapa motisha wanafunzi waliofanya vizuri kila mwaka kwa kuwapatia zawadi ya laptop na fedha taslimu.

Aidha, Dkt. Mwinyi ameahidi kuwafadhili wanafunzi sitini ngazi ya shahada ya kwanza waliofaulu kidato cha sita kwa daraja la kwanza kutoka Unguja na Pemba.
Aidha, Dkt. Mwinyi ameahidi kuwafadhili wanafunzi sitini waliofaulu kwa daraja la kwanza katika mtihani wa kidato cha sita kutoka Unguja na Pemba, ili kuendeleza masomo yao katika ngazi ya shahada ya kwanza.
Rais Dkt. Mwinyi alieleza kuwa Serikali itaendelea kuajiri walimu wa masomo ya sayansi na kuboresha maslahi ya walimu wote.
Halikadhalika, Dkt. Mwinyi amesema Serikali itajenga skuli za ghorofa za msingi na sekondari pamoja na kukarabati zile za zamani.
Vilevile, Serikali itaongeza fedha kila mwaka kusaidia udhamini wa wanafunzi wanaoendelea na masomo ya elimu ya juu.
Rais Dkt. Mwinyi amefahamisha kuwa ni mara ya kwanza Pemba kuweka historia kwa kuondosha daraja la sifuri katika matokeo ya kidato cha sita mwaka 2024.
