MBEYA-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kukuza sekta za uzalishaji ikiwemo Kilimo, Mifugo na uvuvi kwa lengo la kuzalisha kwa tija na kuongeza fursa za ajira katika sekta hiyo.
Amesema,katika kutekeleza hilo, Serikali imeongeza bajeti ya sekta hiyo ambapo Wizara ya Kilimo bajeti imeongezeka kutoka bilioni 294 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 hadi trilioni 1.3 mwaka wa fedha 2024/2025.
Mhe. Ridhiwani amesema hayo Agosti 8, 2024 jijini Mbeya katika Viwanja vya John Mwakangale wakati wa kilele cha Maonesho na sherehe za Wakulima (Nanenane) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.
Tags
Habari
Maonesho ya Nanenane
Ridhiwani Jakaya Mrisho Kikwete
Ridhiwani Kikwete
Wizara ya Kazi na Ajira