DODOMA-Serikali imesema inaendelea na utaratibu wa ujenzi wa barabara ya Masasi –Nachingwea- Liwale yenye urefu wa kilomita 175 kwa awamu ili kuendelea kurahisisha shughuli za kiuchumi na biashara kwa wananchi.

“Mhe. Spika naomba nimhakikishie Mhe. Mbunge kwamba taratibu za ujenzi wa barabara hiyo zinafanyika kwa awamu kutokana na upatikanaji wa fedha,”amesema Naibu Waziri Kasekenya.
Katika hatua nyingine, Serikali imetenga fedha kiasi cha shilingi Milioni 500 kwa ajili ya usanifu na matengenezo ya barabara zilizoathiriwa na mvua katika kipindi cha mwaka 2024 - 2025 ikiwemo barabara ya Kongowe –Mjimwema Bhadi Kivukoni kilomita 25.
Naibu waziri Kasekenya alikuwa akijibu swali la Mbunge Viti Maalum Mariam Kisangi alietaka kujua ni lini Serikali itakarabati barabara ya Kongowe-Mjimwema iliyoathiriwa na mvua za El- Nino.