MOROGORO-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali imejipanga kurejesha ile hadhi ya kihistoria ya Mkoa wa Morogoro kuwa mkoa wa viwanda kwa kufufua viwanda na kuvutia uwekezaji mpya.
Rais Dkt. Samia ameyasema hayo wakati akihutubia wakazi wa Mkoa wa Morogoro katika Uwanja wa Jamhuri akihitimisha ziara yake ya siku 5 kwenye mkoa huo.

Katika ziara yake Mkoani humo Rais Samia alitembelea uwekezaji wa upanuzi wa viwanda uliofanywa mkoani humo ikiwemo Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa, na Kiwanda cha Sukari cha Kilombero.
Pamoja na mambo mengine, Rais Samia amesema kuwa upanuzi huo wa uwekezaji kwenye viwanda unampa imani kuwa ifikapo mwaka 2025/2026 Tanzania itakuwakatika
nafasi nzuri ya kujihakikishia uzalishaji wa sukari kukidhi mahitaji yake.

Mapema leo, Rais Samia alizindua Kiwanda cha Sigara cha Serengeti (SCC) katika eneo la Kiwanda cha Uchakataji Tumbaku cha Mkwawa
(MTPL) ambapo amepongezi uwekezaji huo ambao utakamilika Juni 2025, na kuzalisha ajira mpya 12,000 mkoani Morogoro.