Serikali yashauriwa kuanzisha Kliniki ya Fedha

NA JOSEPHINE MAJULA
WF

SERIKALI kupitia Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Taasisi za kifedha ikiwemo Benki Kuu, Taasisi za Uwekezaji na Bima zimeshauriwa kuanzisha kliniki ya elimu ya fedha kipindi cha mavuno ili kuwafikia wakulima katika maeneo yao ya uzalishaji.
Mkazi wa Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, Bw. Cosmas Rashid, akisoma kipeperushi chenye taarifa kuhusu mikopo wakati wa semina ya elimu ya fedha iliyotolewa na Wizara ya Fedha ambapo mada mbalimbali zilifundishwa ikiwemo kujiwekea akiba, mikopo, uwekezaji katika ukumbi wa Halmashauri hiyo mkoani Lindi.

Ushauri huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, Bw. George Mbesigwe, alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha ambayo ipo mkoani humo kutoa elimu ya fedha kwa wananchi wa makundi mbalimbali wakiwemo wakulima, wafanyabiashara na wanafunzi.
Baadhi ya Wakazi wa Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi walioshiriki semina ya elimu ya fedha wakiangalia filamu yenye mada mbalimbali ikiwemo utunzaji wa akiba, uwekezaji, na nyinginezo iliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo mkoani Lindi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, Bw. George Mbesigwe, akizungumza wakati wa semina ya elimu ya fedha iliyotolewa na Wizara ya Fedha ambapo mada mbalimbali zilifundishwa ikiwemo kujiwekea akiba, mikopo, uwekezaji katika ukumbi wa Halmashauri hiyo mkoani humo.
Mkazi wa Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, Bi. Bahati Mng’onye, akitoa ushauri kwa Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha iliyopo mkoani Lindi kutoa elimu ya fedha kwa wananchi wa makundi mbalimbali.

"Kipindi cha mavuno huku kwetu ndo kipindi ambacho wananchi wanakua na fedha, hivyo elimu hii ikitolewa wakati wa mavuno itasaidia wakulima kuhamasika kufungua akaunti benki, kufanya uwekezaji kupitia Taasisi za Uwekezaji au kukata Bima ya mazao kwakuwa zitakua zimefika katika eneo husika la mavuno," alisema Bw. Mbesigwe.

Aliongeza kuwa uhitaji wa elimu ya fedha kwa wananchi ni mkubwa hivyo ni vyema zoezi hilo likawa endelevu ili kuhakikisha linawafikia wananchi wengi ili waweze kupanga matumizi sahihi ya fedha zao.
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, Bw. Edward Mbaruku, akiwashukuru Wananchi wa Ruangwa, waliojitokeza kupata elimu ya masuala ya fedha katika semina hiyo mada mbalimbali zilifundishwa ikiwemo uwekezaji, mikopo na akiba.

Naye Afisa Maendeleo wa Wilaya ya Ruangwa, Bw. Edward Mbaruku, aliahidi kuendelea kuwahamasisha wananchi wa Halmashauri hiyo kujenga mazoea ya kujiwekea akiba, kukopa katika Taasisi rasmi kuepuka migogoro lakini pia kusajili vikundi ili waweze kutambulika na Serikali na kuwa na sifa yakupata mikopo na fursa nyingine zinazotolewa na Serikali kupitia vikundi.Afisa Msimamizi Mkuu wa Fedha, Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha Bw. Salim Khalfan Kimaro, akiitambulisha Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha ambayo ipo mkoani Lindi kutoa elimu ya fedha, kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Bw. George Mbesigwe (katikati) na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Ruangwa Bw. Rashid Namkulala.

Naye Afisa Msimamizi Mkuu wa Fedha, Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha Bw. Salim Khalfan Kimaro, aliwashukuru wananchi wa Ruangwa kwa ushirikiano waliouonesha wakati wa semina kwa kuuliza maswali na kutoa ushauri ambao utazingatiwa awamu nyingine ya zoezi la utoaji elimu ya fedha.Afisa Mchambuzi Hesabu Mwandamizi, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Bi. Mariam Omari Mtunguja, akizungumza wakati wa semina ya utoaji ya elimu ya masuala ya fedha kwa Wakazi wa Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, ambapo mada mbalimbali zilifundishwa ikiwemo uwekezaji, mikopo na akiba.

“Sisi kama Wizara ya Fedha tunaahidi kuendelea kutoa elimu ya fedha kwa wananchi wa makundi mbalimbali ili kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na elimu hii muhimu kwa kuwa itamsaidia kupanga bajeti, kujiwekea akiba na kufanya uwekezaji na kujikwamua kiuchumi,”alisema Bw. Kimaro.
Mchumi kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Glory Uisso, akizungumza na baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, baada ya kumalizika kwa semina ya elimu ya fedha iliyotolewa na Wizara ya Fedha ambapo mada mbalimbali zilifundishwa ikiwemo kujiwekea akiba, mikopo, uwekezaji katika ukumbi wa Halmashauri hiyo mkoani humo.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WF, Lindi).

Katika zoezi la kutoa elimu kwa Wananchi, Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha imeambatana na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC), wakiwa mkoani Lindi watatoa elimu hiyo katika Wilaya ya Liwale, Nachingwea, Mtama, Ruangwa, Kilwa na Manispaa ya Lindi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news