Serikali yazitaka taasisi za umma kuwa na programu maalum ya michezo

NA VERONICA MWAFISI

KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka amezielekeza Ofisi za Umma kuwa na programu maalum ya michezo kwa Watumishi wa Umma ili kuimarisha afya zao na kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kwa ustawi wa taifa.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka (wa kwanza kushoto) akifanya mazoezi ya viungo wakati wa Bonanza la Michezo ya SHIMIWI lililofanyika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Wa pili kutoka kushoto ni Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi. Wengine ni Viongozi wa Serikali waliohudhuria bonanza hilo.

Balozi Dkt. Kusiluka amesema hayo Agosti 10, 2024 katika Bonanza la Michezo ya SHIMIWI lililofanyika katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma ikiwa ni maandalizi ya michezo ya SHIMIWI inayotarajia kuanza tarehe 18 Septemba hadi 05 Oktoba, 2024 mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka (aliyesimama) akizungumza na Watumishi wa Umma walioshiriki katika Bonanza la Michezo ya SHIMIWI lililofanyika leo katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Bonanza la Michezo ya SHIMIWI lililofanyika leo katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akitoa salamu za ofisi yake wakati wa Bonanza la Michezo ya SHIMIWI lililofanyika leo katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Balozi Dkt. Kusiluka ametoa rai kwa Wizara na taasisi zote za umma kutenga bajeti na muda kwa ajili ya michezo kwa watumishi wa umma ili waweze kushiriki kwa lengo la kuimarisha afya zao, kudumisha umoja na ushirikiano.

Aidha, Dkt. Kusiluka amempongeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Gerson Msigwa kwa kushiriki katika maandalizi ya bonanza hilo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi amesema kuwa agizo la Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka la kutaka Ofisi za Umma kuwa na programu maalum ya michezo kwa watumishi wa umma ni jambo jema kwani itawahamasisha zaidi kutunza afya zao na kuwawezesha kutekeleza majukumu na kutoa huduma bora kwa wananchi.
Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara, Posho na Marupurupu, Bi. Mariam Mwanilwa (wa kwanza kushoto) pamoja na watumishi wa ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifanya mazoezi ya viungo wakati wa Bonanza la Michezo ya SHIMIWI lililofanyika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Katibu Mkuu-UTUMSHI, Bw. Juma Mkomi (kushoto) akizungumza jambo na Katibu Mkuu-IKULU, Bw. Mululi Majula Mahendeka (kulia) wakati wa Bonanza la Michezo ya SHIMIWI lililofanyika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Bonanza la Michezo ya SHIMIWI lililofanyika leo katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifanya mazoezi ya viungo wakati wa Bonanza la Michezo ya SHIMIWI lililofanyika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakimsikiliza mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka (hayupo pichani) wakati wa Bonanza la Michezo SHIMIWI lililofanyika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (aliyevaa traki nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi na Watumishi wa ofisi yake mara baada ya kumalizika kwa Bonanza la Michezo la SHIMIWI lililofanyika katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (aliyevaa traki nyeusi) akifurahia jambo na Wakurugenzi na Watumishi wa ofisi yake mara baada ya kuhitimisha Bonanza la Michezo ya SHIMIWI lililofanyika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Vilevile, Bw. Mkomi ameongeza kuwa ofisi yake imekuwa ikishiriki kliniki za afya kwa watumishi wa umma ambapo hivi karibuni ilishirikiana na Hospitali ya Benjamin Mkapa katika kambi maalum ya zoezi la upimaji afya wa hiari katika maeneo ya ofisi za Serikali Mtumba lengo likiwa kuimarisha afya za watumishi wa umma.

Viongozi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wameshiriki katika bonanza hilo ambalo hufanyika kila mwaka, na Kaulimbiu ya mwaka huu ni “Michezo Huboresha Utendaji kazi, Shiriki Uchaguzi wa serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news