DODOMA-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali zote mbili zitaendelea kudumisha uhuru wa kuabudu kwani ni njia muhimu ya kuimarisha umoja miongoni mwa Watanzania.


Wakati huo huo, Askofu Mkuu wa Kanisa la TAG, Barnabas Mtokambali, amemkabidhi Rais Dkt. Mwinyi Tuzo Maalum ya Uongozi Uliotukuka na kuthamini juhudi zake za kuimarisha uchumi wa Zanzibar.
Askofu Mkuu, Barnabas Mtokambali amempongeza Dk. Mwinyi kwa maendeleo makubwa yanayofikiwa na Zanzibar kwani yanaonesha dhamira ya dhati aliyonayo ya kuwatumikia wananchi.

Mara baada ya kumaliza mkutano huo, Rais Dk. Mwinyi alirejea Zanzibar na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi, wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais, Mhe. Suleiman Hemed Abdallah, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.