Shilingi 200,000 zampomza Mtendaji wa Kata mkoani Manyara

MANYARA (Agosti 15, 2024)-mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro ambaye ni Mtendaji wa Kata ya Orkesmet amefikishwa mahakamani na kufunguliwa shauri namba 23073/2024.
Ni kwa makosa ya kujihusisha na vitendo vya rushwa kinyume na kifungu cha 15(1) (a) na (b) vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

Pia ameshtakiwa kwa kosa la kutotimiza wajibu wa kisheria kinyume na kifungu cha 123 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo 2022.

Mshtakiwa huyo katika nyakati tofauti imedaiwa aliomba na kupokea kiasi cha shilingu 200,000 kutoka kwa Thobius Leparoko Moikan ili asimchukulie hatua za kisheria kwa kosa la kulima na kuvuka eneo la barabara ya mtaa.

Shauri tajwa limesomwa mahakamani na mwendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU),Wakili Faustin Mushi mbele ya Mhe. Charles Uissoo ambaye ni Hakimu Mwandamizi Wilaya ya Simanjiro.

Mshtakiwa amekana mashtaka yote na yupo nje kwa dhamana na kesi hiyo itakuja tena mahakamani Agosti 26,2024 kwa ajili ya kusomwa hoja za awali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news