Shirikianeni na wakulima wajifunze kwa vitendo-RC Kunenge

NA DIRAMAKINI

MKUU wa Mkoa wa Pwani,Mheshimiwa Abubakar Kunenge ametembelea Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki yanayohusisha Mikoa ya Pwani, Morogoro, Tanga na Dar es Salaam.
Akiwa kwenye viwanja hivyo Agosti 5,2024 mkuu huyo wa mkoa ametembelea mabanda ya maonesho na vitalu mbalimbali vya mazao ya kilimo na mifugo.

Pia Kunenge amepongeza taasisi za utafiti kwa kufanya tafiti nzuri na amewataka kushirikiana na wakulima ili wajifunze kwa vitendo.Amemshukuru,Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa utoaji wa pembejeo na viuatilifu.

Ameeleza kuwa, kanda hiyo ya Mashariki inakuwa kwa kasi katika kilimo cha biashara na chakula na kuwa wana matunda na vyakula vingi ikiwemo mboga za majani ambapo wakulima wanatumia teknolojia rahisi katika kuhifadhi mazao hayo ili yasiharibike.

Katika hatua nyingine, Kunenge ameendelea kuhimiza matumizi ya nishati mbadala ambapo amewataka wadau wote wanaohusika na utengenenzaji wa nishati hizo kujitangaza zaidi na kushirikiana na Shirika la STAMICO ili kupata masoko na kufikia wananchi.

Aidha,amewataka watalaam kufanya tathimini ya maonesho haya ili kuendelea kuboresha maonesho hayo ili kwenda pamoja na maono ya Mheshimiwa Rais ikiwemo lile la kulisha Dunia.

Ameyataka pia makampuni yaliyoshiriki maonesho hayo kutumia wanaufaika wa huduma na teknolojia zao kueleza mafanikio na tija walizopata na amewasisitiza wataalam hao kutoa mafanikio yenye tija yanayogusa wananchi na watu wa kawaida.

Wakati huo huo, RC Kunenge amezitaka halmashauri kuangalia uwezekano wa kutoa mikopo ya vijana,wanawake na wenyewe ulemavu kwa vikundi kwa kutoa mikopo kwa ajili shughuli za utengenezaji wa nishati mbadala kwa kutumia mabaki ya miwa.

Maonesho ya Nane Nane 2024 yanafanyika katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini jijini Mbeya kwenye Uwanja wa John Mwakangale; Kanda ya Mashariki mjini Morogoro kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere;

Kanda ya Kusini mjini Lindi kwenye Viwanja vya Ngongo; Kanda ya Ziwa Magharibi jijini Mwanza katika Viwanja vya Nyamhongolo; Kanda ya Ziwa Mashariki mkoani Simiyu katika Viwanja vya Nyakabindi;

Kanda ya Kaskazini jijini Arusha kwenye Viwanja vya Themi; na Kanda ya Magharibi mjini Tabora kwenye Viwanja vya Fatma Mwasa.

Kauli mbiu ya Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa Nane Nane 2024 ni "Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi".

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news