Sillo azitaka NIDA na Uhamiaji kushirikiana

KAGERA-Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhe. Daniel Sillo amezitaka Idara mbili zilizopo chini ya Wizara yake ambazo ni Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kagera kushirikiana ili kuboresha utendaji kazi.
Kauli hiyo ameitoa wilayani Muleba mkoani Kagera katika Mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Balozi Dkt. Emanuel Nchimbi ambapo amewataka kushirikiana na kufanya kazi kwa weledi na uadilifu ili kuwezesha upatikanaji wa Vitambulisho vya Taifa kwa wakati.
"Niwaombe Uhamiaji na NIDA shirikianeni katika suala zima la utambuzi na usajili wa wananchi ili kuharakisha upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa kwa Wananchi wenye sifa. Sitegemei kuona jambo lolote kukwamisha Vitambulisho hivyo bila sababu za msingi,"amesema Mhe. Sillo.
Ametoa agizo hilo ikiwa ni maelekezo ya Katibu Mkuu wa Chama akiwa Wilayani Ngara Mkoani Kagera na kuelezwa na Wananchi kuwa bado wanachangamoto ya upatikanaji wa Vitambulisho vya Taifa.
Hata hivyo, amemuelekeza Afisa Usajili wa NIDA kuwa katika Mkoa wa Kagera bado kuna Vitambulisho 78,766 havichukuliwa na Wananchi ambapo ametoa wito kwa Wananchi kwenda kuchukua Vitambulisho hivyo katika Wilaya, Kata na Vijiji vilivyopo karibu nao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news