Simba nyanyukeni, songeni mbele-Rais Dkt.Samia

DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan ameongea na Wanasimba moja kwa moja.
Ni baada ya Agosti 3,2024 kumpigia simu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa,Utamaduni na Michezo, Gerson Msigwa akiwa ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Aidha,Rais Dkt.Samia amewapongeza Simba SC kwa kuendelea kulifanya Tamasha la Simba Day kuwa bora kila mwaka.

“Hongereni sana Wanasimba kwa Tamasha bora la Simba Day. Mwaka jana tulikuwa wote,lakini leo imeshindikana kutokana na ratiba kuwa ngumu nimeshindwa kuwa hapo.

“Nafahamu msimu uliopita hamkuwa bora sana, lakini yaliyopita si ndwele, nyanyukeni songeni mbele,” amesema Dkt. Samia

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news