ADDIS ABABA-Mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kati ya Simba Queens dhidi ya FAD Djibouti uliokuwa upigwe kesho sasa utafanyika Jumatatu.

Kwa mujibunwa taarifa kutoka Simba,mabadiliko hayo ya ratiba yanakipa nafasi kikosi chao kuendelea kuzoea hali ya hewa ya Ethiopia ambayo ni baridi.
Aidha,morali za wachezaji zipo juu na wanaendelea na programu za mazoezi chini ya Kocha Juma Mgunda na wasaidizi wake.