Simba Queens kumenyana na FAD Djibouti wiki ijayo

ADDIS ABABA-Mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kati ya Simba Queens dhidi ya FAD Djibouti uliokuwa upigwe kesho sasa utafanyika Jumatatu.
Michuano hiyo ambayo inashirikisha timu nane kutoka kwenye makundi mawili imeanza kutimua vumbi leo katika Uwanja wa Abebe Bikila nchini Ethiopia.

Kwa mujibunwa taarifa kutoka Simba,mabadiliko hayo ya ratiba yanakipa nafasi kikosi chao kuendelea kuzoea hali ya hewa ya Ethiopia ambayo ni baridi.

Aidha,morali za wachezaji zipo juu na wanaendelea na programu za mazoezi chini ya Kocha Juma Mgunda na wasaidizi wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news