Simba Queens wapo tayari kuivaa Polisi Bullets

ADDIS ABABA-Simba Queens imefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Brimo Meda kujiandaa na mchezo wa kesho Ligi ya Mabingwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) wa Nusu Fainali dhidi ya Polisi Bullets kutoka Kenya.
Kwa mujibu wa uongozi wa timu hiyo, mchezo huo wa Nusu Fainali ambao wanatarajia utakuwa mgumu utapigwa kesho saa tano asubuhi katika Uwanja wa Abebe Bikila.

Aidha,wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na hakuna aliyepata maumivu ambayo yatamfanya kuukosa mchezo huo muhimu ambao lengo lao ni kushinda ili kutinga fainali.

Pia,morali za wachezaji zipo juu na kila mmoja yupo tayari kuhakikisha anaipambania timu kufikia malengo yake.

Ikumbukwe, Agosti 23,2024 Uwanja wa Abebe Bikila katika mchezo wao mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) dhidi ya Buyenzi kutoka Burundi uliopigwa Uwanja wa Abebe Bikila ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2.

PVP Buyenzi walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya pili kupitia kwa Rukiya Bizimana baada mpira uliopigwa kuokolewa na mlinda mlango Caroline Rufa kabla ya kumkuta mfungaji.

Jentrix Shikangwa aliwapatia Simba Queens bao la kusawazisha dakika ya saba kwa shuti kali lilomshinda mlinda mlango wa PVP, Adidja Nzeyimana baada ya kupokea pasi ndefu kutoka kwa Ruth Ingosi.

Vivian Corazone aliwapatia bao la pili dakika ya 18 baada kutumia vizuri makosa ya walinzi wa PVP na kuachia shuti kali lililomshinda mlinda mlango.

PVP walisawazisha bao hilo dakika ya 61 kufuatia mlinzi Daniela Ngoyi kujifunga wakati akijaribu kuokoa mpira wa kona uliopigwa na Channy Nsabiyumva.

Kocha Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwatoa Jentirx Shikangwa, Saiki Mary, Elizabeth Wambui, Violeth Nicholas na Precious Christopher na kuwaingiza Asha Rashid, Dotto Evarist, Amina Bilal, Jackline Albert na Asha Djafar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news