Simba Queens yatolewa nusu fainali CECAFA

ADDIS SABABA-Simba Queens imeshindwa kutinga fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) baada ya kupoteza kwa mabao 3-2 dhidi ya Polisi Bullets kutoka Kenya.
Mchezo huo ulikuwa mkali muda wote huku timu zikishambuliana kwa zamu huku zikitaka kupata bao la mapema ili kujiweka kwenye nafasi nzuri.

Polisi walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 30 baada ya Lucy Jira kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango Caroline Rufa.

Vivian Corazone aliwapatia Simba Queens bao la kusawazisha dakika ya 39 baada ya kutumia vizuri makosa ya mlinda mlango wa Polisi Kwasi.

Aidha,Vivian aliwapatia bao la pili dakika ya 56 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Elizabeth Wambui.

Dakika ya 63 Diana Mwihaki aliisawazishia Polisi kwa kichwa mpira wa adhabu ulopigwa na Lydia Akoth.

Vile vile dakika ya 82 Rebecca Okwaro aliwapatia Polisi bao la tatu dakika ya 82 na kuwapeleka fainali.

Kocha Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwatoa Preicous Christopher, Ritticia Nabbosa na Violeth Nicholas na kuwaingiza Asha Djafar, Asha Mwalala na Esther Mayala.

Matokeo hayo yanaifanya Simba Queens kukutana na mshindi kati ya Kawempe Muslim na CBE katika mchezo wa kumtamfuta mshindi wa tatu.

Katika mtanange huo uliopigwa Agosti 26,2024 uwanja wa Abebe Bikila saa tano asubuhi,Kocha wa Simba Queens alipanga kikosi kama ifuatavyo;

Caroline Rufa (18), Fatuma Issa (5), Ruth Ingosi (20), Daniela Ngoyi (22), Violeth Nicholaus (26), Ritticia Nabbosa (13), Elizabeth Wambui (4), Vivian Corazone (17), Jentrix Shikangwa (25), Precious Christopher (8), Amina Bilali (11).

Wachezaji wa Akiba:

Gelwa Yonah (21), Wincate Kaari (12), Easther Mayala (23), Saiki Mary (19), Jackline Albert (16), Asha Djafari (24), Mwanahamisi Omary (7), Shelda Boniface (9), Asha Rashid (14).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news