DAR-Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam kati ya Septemba 13 hadi 15 itacheza mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho barani Afrika hatua ya kwanza dhidi ya Al Ahly Tripoli kutoka Libya.
Mchezo huo utakuwa wa ugenini ambao utapigwa nchini Libya kabla ya mechi ya marudiano ambayo itapigwa jijini Dar es Salaam, kati ya Septemba 20 hadi 22.
Al Ahly Tripoli imefika hatua hiyo baada ya kuitoa Uhamiaji kutoka Zanzibar kwa jumla ya mabao 5-1.
Simba SC ni miongoni mwa timu chache zenye alama nyingi Afrika ambazo hazikuanzia hatua ya awali.
Mshindi wa jumla kati ya Simba SC na Al Ahly Tripoli ataingia moja kwa moja katika hatua ya makundi ya michuano hiyo.