Simba SC yapania kuwapa furaha mashabiki wake

DAR-Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Fadlu Davids amesema, mchezo wa kesho dhidi ya APR wa kilele cha Simba Day utakuwa mzuri ambao utawapa picha kuelekea msimu ujao wa mashindano.
Kocha Fadlu amesema, itakuwa jambo zuri kupata ushindi kwenye mchezo wa kesho kutokana na kuwa na sherehe, lakini atawapa nafasi wachezaji wote ili kuzoea mazingira ya kucheza katika wingi wa mashabiki.

Pia,Kocha Fadlu ameupongeza uongozi wa klabu kwa kusajili wachezaji bora wenye umri mdogo ambao wana nguvu na ari ya kuipambania Simba kufikia malengo waliyojiwekea.

“Kikosi kipo kwenye hali nzuri, mchezo wa kesho utakuwa kipimo bora kwetu, tunafahamu mashabiki watajitokeza kwa wingi uwanjani nasi tunaona itakuwa jambo zuri kuwapa furaha ya ushindi.”

“Ninafahamu Simba haijatwaa taji la ligi kwa miaka mitatu lakini safari hii tuna timu bora ambayo najivunia kuwa itatupeleka kwenye malengo tuliyojiwekea,” amesema Kocha Fadlu.

Kwa upande wake nahodha wa timu, Mohamed Hussein (Zimbwe Jr) amewatoa hofu Wanasimba na kuwaambia kuwa,wana timu imara ya ushindani na kesho wataanza kupata furaha waliyokuwa wanaisubiri.

“Tupo tayari kwa mchezo wa kesho, tunajua kuwa ni sikukuu ya Wanasimba na tiketi zimeisha siku tatu kabla kwahiyo wachezaji tunajua tuna jambo kubwa la kufanya,” amesema Nahodha huyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news