Singida Black Stars yaonja kileleni kwa mabao 3-1, Simba SC yaishusha fasta

NA DIRAMAKINI

LIGI Kuu ya NBC Tanzania Bara msimu wa 2024/2025 imeendelea kupamba moto, ambapo Singida Black Stars imeachia kichapo cha mabao 3-1 kwa KenGold.
Ni kupitia mtanange uliopigwa leo Agosti 18,2028 saa 8:00 mchana katika dimba la Sokoine mkoani Mbeya.

Mabao ya Singida Black Stars yamefungwa na Emmanuel Keyekeh dakika ya 41,Elvis Baranga Rupia dakika ya 62 na Camara Damaro dakika ya 81.


Aidha, kwa upande wa KenGold ambao walikuwa wenyeji lilifungwa na Joshua dakika ya 68 ya kipindi cha pili cha mtanange huo.

Matokeo ya Singida Black Stars yaliwapandisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC kwa muda kabla ya matokeo ya mchezo wa pili uliozikutanisha Simba SC dhidi ya Tabora United.


Simba SC iliwakaribisha Tabora United katika uwanja wa KMC saa 10:15 jioni na kumalizika kwa Simba SC kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 yakifungwa na Che Malone, Valentino Mashaka Kusengama na Awesu Awesu.

Kwa matokeo hayo Simba imepanda kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikitofautiana kwa idadi ya mabao na Singida Black Stars na Mashujaa ambao wote wana alama tatu kwa sasa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news