Singida na Dodoma yakaribisha wawekezaji mbalimbali

DODOMA-Mikoa ya Singida na Dodoma imewakaribisha wawekezaji wakubwa na wadogo kwenda kuwekeza katika mikoa hiyo kwa sababu tayari imeweka mazingira mazuri kwa mtu au Kampuni kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo Viwanda, Kilimo, Madini na Utalii.
Wakizungumza kwenye Kongamano la Uwekezaji lililojumuisha wawekezaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi katika Maonesho ya Kimataifa ya Nane Nane yanayofanyika jijini Dodoma, Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule na Mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego wamewahakikishia wawekeza wakaowekeza kwenye mikoa yao kuwa watakuwa wamechagua mikoa sahihi ya kuwekeza kwa sababu ipo kati kati ya nchi na miundombinu ya usafiri ni mizuri.
Wakuu hao wa Mikoa wamesema kuwa wanataka kuona mikoa ya Singida na Dodoma inakuwa mikoa ya kwanza nchini yenye idadi kubwa ya wawekezaji kama hatua ya kukuza uchumi wa wananchi na wa Taifa kwa ujumla kupitia fursa za uwekezaji.

Tupo tayari na tunawakabiribisha mje kuwekeza kwenye mikoa yetu kwa sababu tayari Serikali imeweka mazingira mazuri bora ya uwekezaji ikilinganishwa na hapo awali, wamesisitiza wakuu hao wa mikoa.
Kwa upande wake,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo akizungumza wakati wa kufungua Kongamano hilo la uwekezaji, amesema kwa Serikali inaendelea kuchukua hatua stahiki katika uimarishaji wa uwekezaji hasa katika sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa sababu zinamchango mkubwa katika kuinua uchumi wa wananchi na wa Taifa kwa ujumla.

Profesa Mkumbo amesema kwa sasa Serikali imefanya marekebisho makubwa ya sera na sheria za uwekezaji nia ikiwa ni kuondoa vitendo vya ukiritimba ambavyo vilikuwa vinakwamisha wawekezaji wengi kuja kuwekeza katika maeneo mbalimbali nchini.
Amesema mchakato huo unaenda sambamba na upunguzaji wa utitiri wa baadhi ya Taasisi mbalimbali za umma ambazo zingine ni legevu na zimekuwa kiwango katika masuala ya uwekezaji.Kongamano hilo limehudhuriwa pia na Waziri Mkuu Mstaafu na Balozi wa Kilimo nchini Mizengo Pinda.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news