Sitomuangusha Mheshimiwa Rais Dkt.Samia katika majukumu haya-Waziri Ridhiwani Kikwete

NA GODFREY NNKO

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu),Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumkabidhi wizara hiyo, huku akiahidi hatomuangusha.
Mheshimiwa Waziri Ridhiwani ameyasema hayo kupitia mahojiano katika Kipindi cha Dakika 45 cha ITV. Mahojiano ambayo ni ya kwanza kufanya na chombo cha habari tangu Mheshimiwa Rais Dkt.Samia ampangie majukumu hayo mapya katika wizara.

Hivi karibuni, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hasaan alimteua na kumuapisha Ridhiwani Kikwete kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) akichukua nafasi ya Deogratius John Ndejembi ambaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Kabla ya uteuzi huo, Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete alikuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

"Pia, nitumie nafasi hii kumshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kuniona, kwa sababu wabunge wako wengi, manaibu waziri tulikuwa wengi.

"Lakini akaona katika manaibu waziri tulionao, huyu ninadhani sasa anaweza kupanda nafasi hii akatusaidia katika jambo hili.

"Kwa hiyo, ninataka kupitia nafasi ambayo nimepata ambayo ninaweza kusema ni chombo cha kwanza kupata fursa ya kuongea nacho kumshukuru sana Mheshimiwa Rais na mbele ya umma nimuahidi kwamba sitomuangusha katika majukumu haya ambayo amenikabidhi."

Mipango aliyonayo

"Mipango iko ya namna nyingi, kwa sababu, kwanza mimi nilikuwa Ofisi ya Rais-Utumishi ambapo kule ambacho nilikuwa ninakifanya na kitu ambacho ninafanya hapa, ni vitu viwili ambavyo kwa namna moja au nyingine vinafanana kwa kisura ya nje, lakini kisura ya ndani ni vitu ambavyo vinafanya kazi kwa kutegemeana.

"Lakini, mipango mikubwa ambayo tuliyo nayo sisi ni ile miongozo ambayo tunayo kwenye ofisi.Unajua, unapochaguliwa kuwa Waziri katika wizara yoyote, kwanza lazima ile wizara ina programu zake.

"Kwamba, bwana hapa kuna hiki, kuna hiki na kuna hiki. Mimi jukumu langu kubwa ambalo ninalo ukiachilia yaliyopo kwenye kitabu ni kwenda. Endelea kutazama mahojiano hapa chini; 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news