Soya ni fursa kwa ardhi ya Dodoma

DODOMA-Kitalu cha zao la soya cha kampuni ya Longping kutoka nchi ya Brazil kimetia fora katika Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane 2024 na kudhihirisha kuwa Dodoma haina ukame, bali ina ardhi yenye rutuba kwa shughuli za kilimo cha zao la soya.
Hayo yanebainika hivi karibuni wakati wa mahojiano na Bw. Michael Bishubo, mwakilishi kutoka katika kampuni ya Longping ambaye ameeleza kuwa kampuni hiyo inashiriki katika Maonesho ili kutoa hamasa kwa wananchi wa Dodoma juu ya kilimo cha soya.

Aidha, amesema kuwa kwa sasa wamejiandaa kulima maeneo mbalimbali likiwemo shamba lao la Lwasho lililopo Songwe ambalo wamelima kwa mara ya kwanza na wamepata mazao ya kutosha kwa wastani wa tani 2.7 kwa ekari ambapo mavuno yake yameuzwa hapahapa nchini.

“Soko la zao la soya linazidi kushamiri na kuimarika hapa nchini na duniani, hivyo kampuni ya Longping imejipanga kuanza kulima soya mkoani Dodoma katika eneo la Ndogowe; ikiwa ni pamoja na kununua soya zitakazozalishwa katika shamba la Vijana wa BBT la Ndogowe.”

Kampuni hiyo pia inaendeleza shamba la hekta 10,000 Mkulazi, Morogoro.

Zao la soya kwa kutumia mbegu ya aina ya MG3801 linastawi vizuri na kuota karibia maeneo ya Kanda zote za Kilimo kwa muda wa siku 110 hadi 120 tangu kupandwa hadi kuvunwa.

Zao la soya husindikwa na hutoa mafuta, chakula cha binadamu na chakula cha mifugo; huku likiwa ni miongoni mwa mazao ya jamii ya mikunde yenye protini nyingi.

Wakulima wanahamasishwa kuchangamkia fursa ya kilimo cha zao la soya kwa kuwa soya nyingi inayotumika hapa nchini inatoka nchini Zambia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news