DODOMA-Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Tulia Ackson leo Agosti 27,2024 katika Mkutano wa 16 wa Bunge amemuapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Bw. Hamza Johari.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Tulia Ackson akimuapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Hamza Johari leo Agosti 27,2024 jijini Dodoma.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Bw. Hamza Johari akila kiapo bungeni leo Agosti 27,2024 jijini Dodoma.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Bw. Hamza Johari akimsalimia Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dkt.Doto Biteko baada ya kula kiapo leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu),Mhe. William Lukuvi (kushoto) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Mheshimiwa Hamza Johari wakipitia nyaraka bungeni leo.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Mheshimiwa Hamza Johari akimsalimia Mheshimiwa Kapteni George Huruma Mkuchika ambaye ni Waziri Ofisi ya Rais Kazi Maalum baada ya kula kiapo bungeni leo.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Mheshimiwa Hamza Johari akipitia baadhi ya nyaraka bungeni leo baada ya kula kiapo mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt.Tulia Ackson.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Mheshimiwa Hamza Johari akimsalimia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu), Mhe. William Lukuvi baada ya kula kiapo bungeni leo.