STAMICO kujenga kiwanda cha chumvi Lindi

LINDI-Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) linatarajia kujenga kiwanda cha uchakataji chumvi ghafi mkoani Lindi ambacho kinalenga kutatua changamoto ya upatikanaji wa chumvi hiyo inayozalishwa nchini.
Picha zikionesha muonekano wa Kiwanda cha uchakataji chumvi ghafi ambacho kinajengwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kutatua changamoto ya upatikanaji wa soko wa chumvi ghafi inayozalishwa nchini.

Maandalizi ya ujenzi wa Kiwanda cha chumvi cha mfano kwa ajili wachimbaji wadogo yanaendelea ambapo hadi sasa mtambo wa kuchakata chumvi unaendelea kutengenezwa nchini India.
Kiwanda hicho cha kuchakata chumvi ghafi kitajengwa katika Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi na ujenzi unatarajiwa kuanza mwezi Septemba, 2024.
Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa ziara yake katika mikoa ya Kusini mwaka 2023 aliielekeza STAMICO kupitia Wizara ya Madini kuhakikisha inasaidia upatikanaji wa soko la chumvi ghafi inayozalishwa na wazalishaji wa ndani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news