DAR-Taarifa ya thamani ya mifuko ya uwekezaji Julai 31,2024. Taarifa hii hutolewa kila siku kupitia tovuti ya www.uttamis.co.tz
🔻Kupitia taarifa hii utafahamu yafutayo;
🔶Thamani ya mfuko ;
Ni kiasi cha pesa kilichowekezwa katika mfuko husika.( Fund size)
🔶Thamani ya kipande ;
Inaonyesha bei halisi ya kipande (Current unit price) kwa mfuko husika
🔶Bei ya kununua;
Ni bei halisi ambayo mwekezaji atanunua vipande kutoka UTT AMIS kwa wakati husika pindi anapowekeza pesa zake
🔶Bei ya kuuza;
Ni bei halisi ya ambayo mwekezaji atauza vipande vyake wakati husika pindi anapotoa pesa zake kutoka katika akaunti yake
ya uwekezaji
✳️Kumbuka👇
Thamani ya kipande hubadilika kulingana hali ya masoko.
✳️Mwekezaji atakuwa ananunua vipande kutoka UTT AMIS pindi anapowekeza pesa zake na;
✳️Mwekezaji atakuwa anamuuzia vipande UTT AMIS pindi anapotoa pesa zake
🤷♂️Sasa unaweza kutoa pesa chini 2,000,000/- kupitia huduma ya SimInvest. Bonyeza *150*82# kisha fuata maelekezo
Au:
📞Tupigie bure kwa namba:
0800 112020 kwa taarifa zaidi.